MAKAMU wa rais wa klabu ya Barcelona, Carles Vilarrubi amedai kuwa timu hiyo ilikabiliwa na mtikisiko wa kiuchumi kwasababu Real Madrid waliwalazimisha kumsajili Neymar mapema zaidi ya walivyopanga. Hivi karibuni sakata la usajili wa mchezaji huyo lilipelekea Barcelona kufunguka na kuthibitisha kuwa walikuwa tayari wamemsajili nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwaka mmoja kabla ya kutangazwa rasmi. Vilarrubi amkiri kuwa ushindani wa kutaka kuwazidi wapinzani wao katika kumsajili mchezaji huyo uliwaacha katika nafasi mbaya kiuchumi lakini alipendekeza Madrid ndio haswa waliwalazimisha kufanya hivyo. Makamu huyo amesema klabu ilifikia makubaliano ya awali na nyota huyo ili waweze kumsajili kwa msimu wa 2014-2015 lakini msukumo kutoka katika klabu nyingine ulipelekea kumchukua nyota huyo mapema kuliko walivyopanga.
No comments:
Post a Comment