Tuesday, May 6, 2014

RODGERS AKATA TAMAA NA UBINGWA.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers ameamua kukata tamaa na kudai kuwa ndoto za timu yake kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu zimeyeyuka baada ya kukubalia kulazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Crystal Palace. Liverpool walishindwa kulinda lango lao baada ya kupata mabao 3-0 yakuongoza katika Uwanja wa Slehurst Park na sasa wako kileleni mwa msimamo wa ligi kwa alama moja zaidi ya Manchester City ambao wana mchezo mmoja mkononi na tofauti kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Rodgers amesema hakuna shaka kwamba City watashinda taji hilo baada ya timu yake kushindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa jana. Mara baada ya mchezo huo wachezaji wengi wa Liverpool walionekana kutoamini kilichotokea huku mshambuliaji nyota Luis Suarez akishindwa kujizuia na kumwaga machozi hadharani huku akibembelezwa na nahodha Steven Gerrard.

No comments:

Post a Comment