KIUNGO wa klabu ya Arsenal, Abou Diaby amebainisha kuwa alifikiria kustaafu kufuatia majeruhi ya muda mrefu ya goti yanamuandama. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa, ambaye amekaa nje ya uwanja kwa miezi 13 kufuatia kuumia goti, alikuwepo benchi wakati Arsenal ilipoigaragaza West Bromwich kwa bao 1-0 jana. Hiyo imekuwa muonekano wake wa kwanza katika kikosi hicho toka alipoumia mazoezini mwaka jana na kiungo huyo mwenye miaka 27 amebainisha alikuwa akifikiria kustaafu kwa kujiuliza uwezo wake pindi atakaporejea. Hata hivyo, Diaby anajiandaa kuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kitakachojiandaa na mechi mbili za zilizobakia msimu huu ikiwemo fainali ya Kombe la FA.
No comments:
Post a Comment