TIMU ya mawakili wa utetezi katika kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius imeita mashahidi zaidi, wakati wakijaribu kuthibitisha kuwa alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa bahati mbaya. Majirani wawili wa karibu wa Pistorius wamesema leo kuwa walimsikia mwanamume akilia kwa sauti kubwa usiku lilipotokea tukio hilo. Jana watu wengine wawili ambao ndio watu wa kwanza kufika eneo la tukio walielezea jinsi walivyomkuta Pistorius akijaribu kuokoa maisha ya Steenkamp. Mwanariadha huyo anatuhumiwa kumuua Steenkamp usiku wa siku ya wapendanao mwaka uliopita kitu mwenyewe anakanusha na kudai kuwa alimuua kwa bahati mbaya akidhani alivamiwa na majambazi nyumbani kwake.
No comments:
Post a Comment