Tuesday, May 6, 2014

TOTTENHAM YAIOMBA RADHI LIVERPOOL KWA VIDEO YA KEBEHI.


KLABU ya Tottenham Hotspurs imeomba radhi baada ya video ya kukebehi kuanguka kwa Liverpool katika mbio za ubingwa kutokea katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa twitter wa timu hiyo na kudai kuwa watafanyia uchunguzi tukio hilo. Liverpool walitoa sare ya mabao 3-3 nyumbani kwa Crystal Palace jana usiku hivyo kuachia mbio za ubingwa kwa mahasimu wao Manchester City. Kulikuwa na ujumbe uliokuwa ukisomeka kuwa ni Ukatili Lakini Inafurahisha Sana, ulioambatana sambamba na picha za video zikimuonyesha mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez akilia, katika twitter ya timu hiyo. Haraka Spurs waliondoa ujumbe huo na wanaangalia masuala yanayohusiana kiusalama.

No comments:

Post a Comment