RAIS wa timu ya mpira wa kikapu ya Los Angeles Clippers, Andy Roeser amechukua likizo ya muda usiojulikana wakati kukiwa na msukumo wa kuuzwa kwa timu hiyo. Msemaji wa Chama cha Mpira wa Kikapu nchini Marekani-NBA, amesema kuondoka kwa Roeser kutatoa nafasi kwa mmiliki mpya wa timu hiyo kuanza vizuri. Mmiliki wa Clippers Donald Sterling amefungiwa kushiriki masuala yoyote ya mchezo huo maisha baada ya kurekodiwa akitoa kauli za kibaguzi. Jopo la mashauriano la NBA limekubaliana kuanza taratibu za kutafuta mnunuzi wa timu hiyo baada ya aliyekuwepo kukumbwa na sakata hilo. Roeser alikuwa ameajiriwa na Clippers kwa kipindi cha miaka 30 akifanya kazi chini ya Sterling ambaye aliinunua Clippers mwaka 1981.
No comments:
Post a Comment