Tuesday, May 27, 2014

ROAD TO BRAZIL: WAANDAMANAJI WAZONGA BASI LA WCHEZAJI WA BRAZIL WAKIENDA MAZOEZINI.

TIMU ya taifa ya Brazil, imeanza maandalizi yake ya Kombe la Dunia huku kukiwa na maandamano jijini Rio de Janeiro. Basi lililokuwa limebeba wachezaji kuwapeleka katika kambi iliyopo huko Hilltop lilizungukwa na walimu waliokuwa wakiandamana ambao walikuwa wakiimba nyimbo za kupinga michuano hiyo. Baadae tena wakati timu hiyo ilipofika katika kambi yao ya mazoezi huo Granja Comary wachezaji walisalimiwa na mashabiki na waandamanaji zaidi. Maelfu ya wananchi wa Brazil wamekuwa wakiandamana kupinga gharama kubwa zilizotumika kwa ajili ya michuano hiyo inayotarajiwa mwezi ujao. Brazil inakabiliwa na mechi za kirafiki dhidi ya Panama Juni 3 na Serbia Juni 6 kabla ya kucheza mechi yao ya ufunguzi ya michuano hiyo Juni 12 dhidi ya Croatia Juni 12 jijini Sao Paulo.

No comments:

Post a Comment