KLABU ya Inter Milan imeamua kusimamisha matumizi ya jezi yenye namba nne mgongoni kwa heshima ya Javier Zanetti na wanatarajia kumteua beki huyo wa kulia aliyestaafu hivi karibu kuwa makamu wa rais wa klabu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili. Mkongwe huyo wa Argentina aliamua kutundika daruga zake rasmi mwaka huu baada ya kuitumikia Inter kwa kipindi cha miaka 19, ambapo alifanikiwa kushinda mataji matano ya Serie A, manne ya Kombe la Italia, taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia. Rais wa klabu hiyo Erick Thohir amebainisha kuwa sasa Inter itaondoa namba aliyokuwa akivaa nyota huyo kwenye jezi zake ili kumpa heshima kwa kipindi alichofanya kazi hapo pamoja na kumpa nafasi hiyo muhimu kwenye timu hiyo. Thohir amesema uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha bodi walichokutana kujadili jinsi ya kumuenzi mkongwe huyo kwa utumishi wake uliotukuka katika timu hiyo.
No comments:
Post a Comment