KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson anatarajia kumshawishi Steven Gerrard kuendelea na kucheza soka la kimataifa mpaka 2016 na kumuacha nahodha huyo wan chi hiyo katika wakati mgumu wa kufanya maamuzi kati ya kuhitajika kwake na klabu na timu ya taifa. Pamoja na Gerrard mwenye umri wa miaka 34 kushinda kung’aa katika michuano ya Kombe la Dunia, thamani ya uzoefu wake katika kikosi inamaanisha Hodgson atahitaji kiungo kuendelea ili wachezaji chipukizi waweze kuiga mfano wake. Huku Frank Lampard akikaribia kutundika daruga zake katika soka la kimataifa, Gerrard anabakia kuwa mmoja wa wachezaji wachache wakongwe waliobakia na Uingereza hatataka kumpoteza ili kutengeneza uwiano kwa kikosi cha wachezaji chipukizi kilichopo. Hata hivyo, Gerrard itabidi aangalie umuhimu wake katika klabu ya Liverpool ambayo ina ratiba ngumu msimu ujao baada ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na nyota amesema atatoa uamuazi baada ya kuzungumza na marafiki zake, familia na kocha wake Brendan Rodgers baada ya Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment