MAKAMU wa raia wa klabu ya Sao Paulo Ataide Gil Guerreiro amedai kuwa kiungo mahiri wa klabu ya AC Milan, Kaka anatarajiwa akujiunga na nao kwa mkopo kabla ya kuhamia katika timu ya Orlando City. Kaka alirejea Milan katika kipindi cha usajili cha majira ya kiangazi mwaka jana baada ya kukaa Real Madrid kwa miaka minne lakini kulikuwa na kipengele katika mkataba wake kinachomruhusu kuondoka kama timu hiyo ikishindwa kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 sasa anapanga kurejea katika timu yake ya kwanza ya sao Paulo lakini kwa mkopo wa kipindi kifupi kabla ya kusaini mkataba wa muda mrefu na timu ya Orlando City inayoshiriki Ligi Kuu nchini Marekani-MLS mwaka 2015. Guerreiro amesema baada ya siku 60 za mazungumzo hatimaye wamefikia makubaliano lakini hakuna chochote rasmi kilichofanyika. Kaka aliibukia katika shule ya soka ya sao Paulo na kuifungia timu hiyo mabao 23 katika mechi 59 alizocheza katika timu hiyo kati ya mwaka 2001 na 2003 na baadae kwenda barani Ulaya kuichezea Milan ambapo aliitumikia kwa miaka sita akifanikiwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa na Serie A.
No comments:
Post a Comment