SHIRIKISHO la Soka Dunia-FIFA linatarajia kuchunguza tuhuma za ubaguzi zinazodaiwa kutolewa na mashabiki wa Ujerumani katika mchezo dhidi ya Ghana ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2 huko Fortaleza. Picha zilionyesha baadhi ya mashabiki wakiwa wamejipaka rangi nyeusi katika nyuso zao katika mitandao ya kijamii, na kuzua mjadala kuwa mashabiki wa timu za Ulaya wanaonyesha tabia za kibaguzi. Kuongezea uzito madai hayo ni tukio la mshabiki mmoja, ambaye aliingia uwanjani akiwa na maandishi kuhusu Nazi wakati wa kipindi cha pili cha mchezo huo. Msemaji wa FIFA amesema siku zote wanachukua ushahidi wowote unaowasilishwa au kuonekana katika kamati yao ya nidhamu na wao ndio wanaokutana kuangalia kama wanaweza kufungua kesi na baadae tume ya nidhamu kutoa maamuzi.
No comments:
Post a Comment