WAKATI Thomas Muller akifunga bao didi ya Marekani na kuipa ushindi Ujerumani wa 1-0 na kuifanya kuongoza kundi G, hakufikia idadi ya mabao manne ambayo yamefungwa na Lionel Messi na Neymar lakini pia ameweka rekodi mpya ya mabao katika hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka huu. Kufikia muda wa kundi H kumalizia mechi zake za mwisho huku Ubelgiji ikishinda bao 1-0 dhidi ya Korea Kusini na sare ya bao 1-1 kati ya Algeria na Urusi ilihitimisha idadi ya mabao 136 yaliyofungwa katika hatua hiyo ikiwa ni mabao sita zaidi ya yale yaliyofungwa katika michuano ya mwaka 2002 iliyofanyika Korea Kusini na Japan. Wachezaji wengine wanaowafuata kwa karibu kwa ufungaji nyota hao ni pamoja na Robin van Persie, Arjen Robben wote wa Uholanzi, Karim Benzema wa Ufaransa, Enner Valencia wa Ecuador, Rodriguez wa Colombia na Shaqiri wa Switzerland ambao wote wamefunga mabao matatu kila mmoja. Wengine waliofunga mabao mawili katika hatua hii ya kwanza ni pamoja na Tim Cahill wa Australia, Mario Mandzukic wa Croatia, Martinez wa Colombia, Dempsey wa Marekani, Wilfried Bony wa Ivory Coast, Andre Ayew wa Ghana, Asamoah Gyan wa Ghana, Musa wa Nigeria na Slimani wa Algeria.
No comments:
Post a Comment