BEKI mahiri wa kimataifa wa Ufaransa, Bacary Sagna amejibu mapigo kwa mashabiki ambao wanamkosoa wakati alipoondoka Arsenal na kwenda Manchester City na kudai kuwa hakuondoka kwasababu ya fedha bali kuinua kiwango chake. Nyota huyo amejiunga rasmi na City baada ya miezi kadhaa ya mvutano kutokana na kukataa ofa ya mkataba mpya Arsenal, kutokana na huu wa sasa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. Na baada ya kuisaidia Ufaransa kuvuka katika hatua ya timu 16 bora, Sagna amejibu tetesi kuwa kilichomfanya aondoke Arsenal ni mshahara na kudai kuwa kwa miaka sita ameitumikia timu hiyo kwa kiwango kimoja cha mshahara. Sagna amesema kwasasa yeye ni mchezaji wa City, lakini anataka kufafanua kuwa hakuondoka Arsenal kwa fedha kwani toka mwaka 2008 ameitumikia timu hiyo bila kuomba nyongeza ya mshahara. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kilichomfanya kuondoka Arsenal ni kuhitaji mabadiliko ili aweze kujiongeza zaidi katika kazi yake hiyo ya soka.
No comments:
Post a Comment