KOCHA wa timu ya taifa ya Honduras, Luis Fernando Suarez ameamua kubwaga manyanga baada ya kushindwa kuipa ushindi nchi hiyo katika mechi zake zote tatu za hatua ya makundi za Kombe la Dunia. Kocha huyo raia wa Colombia ambaye aliivusha Ecuador katika hatua ya timu 16 bora katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006 iliyofanyika nchini Ujerumani amemua kuachia ngazi kufuatia vipigo vitatu alivyopata katika michuano hiyo inayoendelea nchini Brazil. Suarez ambaye amekuwa kocha Honduras toka Machi mwaka 2011 aliomba radhi mashabiki wa soka wa nchi hiyo kwa kushindwa kufanya vyema huku akidai amesikitika kwasababu alikuwa na ndoto katika michuano hii. Kipigo cha mwisho cha Honduras katika michuano hiyo walikipata jana usiku katika mchezo wao dhidi ya Switzerland uliochezwa katika Uwanja wa Amazoni ambapo walifungwa mabao 3-0, yote yakifungwa na Xherdan Shaqiri.
No comments:
Post a Comment