KIUNGO wa kimataifa wa Brazil, Luiz Gustavo amesema kuondoka kwake katika timu ya Bayern Munich na kwenda Wolfsburg kumemsaidia kwa kikubwa kuinua kiwango chake ambacho kilikuwa kikidorora. Gustavo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Brazil katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea ambapo ametengeneza mojawapo ya mabao ambayo yameivusha nchi hiyo katika hatua ya timu 16 bora. Kiungo amesema anakumbuka mambo mengi mazuri wakati akiwa Bayern hivyo kuondoka na kuiacha klabu hiyo halikuwa jambo rahisi lakini ndio ulikuwa mwanzo kwani amekuja kuwa fiti zaidi. Gustavo alitua Bayern akitokea kwa mahasimu wao wa Bundesliga Hoffenheim Januari mwaka 2011 ambapo aliichezea klabu hiyo kwa miaka miwili na nusu kabla ya kocha mpya Pep Guardiola kumruhusu kuondoka katika majira ya kiangazi mwaka jana. Akizungumzia uamuzi wa Guardiola kumruhusu kuondoka, Gustavo amesema kila mtu ana mawazo yake lakini hivi sasa ana furaha mahali alipokuwepo.
No comments:
Post a Comment