KOCHA wa timu ya taifa ya Uholanzi, Louis van Gaal amesema ametumia mapumziko ya kwanza kwa ajili ya kunywa maji katika Kombe la Dunia kubadilisha mbinu katika kikosi chake ambacho kilitoka nyuma na kuifunga Mexico kwa mabao 2-1. Mabao kutoka kwa Wesley Sneijder na Klaas Jan Hunterlaar katika dakika za majeruhi yalitosha kuisaidia Uholanzi kupata nafasi ya kucheza katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Brazil. Van Gaal amesema mara ya kwanza alibadilisha mfumo kutoka 4-3-3 na baadae kutengeneza nafasi nyingi. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa baada ya hapo alihamia katika mpango B na alifanya hivyo katika muda wa mapumziko ya kunywa maji, kwani ndio ilikuwa njia pekee sahihi ya kutumia mwanya huo.A
No comments:
Post a Comment