NGULI wa soka nchini Argentina ameendeleza vita vya na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA baada ya shirikisho hilo kuwataka wachezaji saba wa Costa Rica kwenda kufanyiwa vipimo baada ya kuifunga Italia. Maradona amesema shirikisho hilo limeonyesha kushindwa kuheshimu sheria baada ya kusisitiza kufanywa ka vipimo hivyo. Wachezaji wawili pekee wa Italia ndio waliofanyiwa vipimo baada ya kufungwa na Costa Rica bao 1-0 Ijumaa na kuzima matumaini ya Uingereza ya kufuzu hatua ya makundi. Maradona mwneye umri wa miaka 53 alihoji kama FIFA wamewataka wachezaji saba wa Costa Rica kufanyiwa vipimo kwanini hawakufanya hivyo kwa wachezaji wa Italia. Nguli huyo aliendelea kudai kuwa anavyofahamu yeye ni wachezaji wawili katika kila timu wanaotakiwa kufanyiwa vipimo kama wametumia dawa za kuongeza nguvu baada ya mchezo husika lakini sio saba. Amedai hatua hiyo inaonyesha jinsi gani FIFA wanavyotapatapa kwa kuona timu vigogo zikiyaaga mashindano mapema hivyo kuwafanya kukosa mikataba minono ya matangazo.
No comments:
Post a Comment