KOCHA wa timu ya taifa ya Nigeria, Steven Keshi amesema ulikuwa usiku mzuri kwa timu za Afrika zinazotoka upande wa Magharibi baada ya kikosi chake kuichapa Bosnia-Herzegovina jana usiku na Ghana kutoa sare ya mabao 2-2 na Ujerumani. Akihojiwa Keshi amesema kila mtu ana furaha kwani Ghana wamepata matokeo waliyohitaji na wao wameshinda hivo ni jambo zuri kwa bara la Afrika. Keshi mwenye umri wa miaka 52 pia alipongeza kiwango cha timu yake walichoonyesha katika michuano hiyo kwa kuhakikisha wanalinda lango lao vyema hivyo kuwafanya kucheza mechi ya pili bila kufungwa. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa wanatakiwa kuendelea na juhudi hizo ili kuhakikisha wanafanikiwa kuvuka hatua inayoafuata kwani mchezo wao wa mwisho dhidi ya Argentina anajua hautakuwa rahisi.
No comments:
Post a Comment