Thursday, June 5, 2014

PLATINI AUNGA MKONO SUALA LA KURA KURUDIWA QATAR.

RAIS wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Michel Platini ametaka kura zirudiwe kwa nchi itakayoandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 kama tuhuma za ufisadi dhidi ya Qatar zitathibitishwa. Qatar kwasasa inachunguzwa baada ya gazeti la Sunday Times la Uingereza kuwatuhumu maofisa wa soka kupokea hongo ili kuinga mkono Qatar katika kinyang’anyiro hicho. Platini aliipigia kura Qatar katika uteuzi huo uliofanyika Desemba mwaka 2010 lakini amesema hajutii chochote kwasababu anadhani Shirikisho la Soka Duniani-FIFA lilifanya uchaguzi sahihi. Kamati iliyokuwa ikiongoza kutafuta nafasi ya uenyeji wa michuano hiyo ilikana tuhuma hizo na kudai hawakufanya jambo lolote la kifisadi.

No comments:

Post a Comment