Thursday, June 5, 2014

VIWANGO FIFA: BRAZIL YAJONGEA TARATIBU KATIKA NAFASI YAKE, TANZANIA NAYO YAJITUTUMUA.

BRAZIL imekwea mpaka katika nafasi ya tatu katika viwango vya ubora duniani ikiwa ni vya mwisho kabla ya michuano ya Kombe la Dunia haijaanza kutimua vumbi. Katika viwango hivyo vya kila mwezi ambavyo hutolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Tanzania imekwea kwa nafasi tisa mpaka katika nafasi ya 113 na kuwazidi majirani zao Rwanda walioko katika nafasi ya 116. Nafasi ya kwanza na pili katika orodha hizo imebaki kwa nchi za Hispania na Ujerumani huku nafasi ya nne na tano ikishikiliwa na Ureno na Argentina. Kwa upande wa Afrika Algeria kwasasa ndio wanaongoza wakiwa katika nafasi ya 22 baada ya kuipita Ivory Coast walioporomoka mpaka nafasi ya 23 wakifuatiwa na Misri waliopo katika nafasi ya 36. Wengine ni Ghana ambao wako katika nafasi ya 37 huku tano bora kwa upande wa Afrika ikifungwa na Cape Verde waliopo nafasi ya 39.

No comments:

Post a Comment