KESI ya mauaji ya mwanariadha nyota mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius imeendelea tena leo baada ya kusimamishwa kwa muda ili aweze kufanyiwa vipimo vya akili kwa mara nyingine. Taarifa kutoka kliniki ya magonjwa ya akili alipokuwa akifanyiwa vipimo mwanariadha huyo imedai kuwa Pistorius hakuwa na tatizo lolote kiakili wakati akimuua mpenzi wake. Mawakili wake wa utetezi wamedai kuwa Pistorius hakuwa katika hali yake ya kawaida wakati alipomfyatulia risasi mpenzi wake. Mwanariadha huyo amekata shitaka la kumuua Reeva Steenkamp kwa makusudi na kudai kuwa ilikuwa bahati mbaya wakati alipoingiwa na hofu na kudhani kuwa alikuwa amevamiwa na majambazi. Pande mbili za mashitaka na utetezi zimekuwa taarifa hiyo. Steenkamp mwenye umri wa miaka 29 aliyekuwa mwanamitindo na mwanasheria, alipigwa risasi kipitia mlango wa bafuni katika nyumba ya Pistorius iliyopo jijini Pretoria katika siku ya wapendanao wamaka jana.
No comments:
Post a Comment