MKURUGENZI wa michezo wa klabu ya Bayern Munich, Matthias Sammer amedokeza kuwa mabingwa hao wa Bundesliga wanaweza kufanya usajili zaidi katika kipindi hiki cha kiangazi kufuatia taarifa za kumfuatilia mshambuliaji nyota wa Borussia Dortmund Marco Reus. Bayern tayari wameshawasajili Roberto Lewandowaski, Sebastian Rode na Juan Bernat kiangazi hiki lakini kocha Pep Guardiola bado anataka kuongeza nguvu kidogo katika safu yake ya ushambuliaji na kumekuwa na tetesi za kumhitaji Reus. Akihojiwa Sammer pamoja na kutotaja majina lakini alikiri kuwa wanaweza kuendelea kutafuta wachezaji katika kipindi hiki cha usajili ili kuepusha suala la uchovu kwa wachezaji baada ya kutoka katika michuano ya Kombe la Dunia. Sammer amesema msimu wa Bundesliga ni mrefu na wachezaji wengi wamepata muda mfupi sana wa kupumzika hatua ambayo inaweza kuwasababishia uchovu huko mbele hivyo ni muhimu kuendelea kuangalia aina ya wachezaji wanaoweza kuongeza nguvu ili kuepukana na suala hilo.
No comments:
Post a Comment