Monday, July 21, 2014

MAYWEATHER KUZICHAPA NA PACQUIAO MEI MWAKANI.

HATIMAYE bondia mahiri mwenye mbwembwe nyingi kutoka Marekani, Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wanaweza kupambana Mei mwakani. Kumekuwa tetesi kutoka kwa watu wa karibu wa baba yake Maytweather ambaye alidai kuwa mwanae ambaye hajawahi kupigwa mpaka sasa yuko tayari kupigana na Mfilipino huyo katika linalotarajiw akuingiza fedha nyingi. Kabla ya pambano hilo la Mei Mayweather anatarajiwa kupigana katika pambano la marudiano dhidi ya bondia Marcos Maidana litakalochezwa Septemba 13 mwaka huu. Pamoja na kwamba Mayweather hana hamasa kubwa ya kupigana na Pacquiao lakini ameonekana kuzitamani fedha ambazo zitapatikana kama wawili hao wakipigana.

No comments:

Post a Comment