Monday, July 21, 2014

NEGREDO AVUNJIKA MGUU KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester City, Alvaro Nigredo amethibitika kuwa amevunjika mguu wake utakaomfanya kukaa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa. Ngredo mwenye umri wa miaka 28 aliumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Hearts jana na kuthibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram sambamba na picha ya mguu wake wa kulia ukiwa na bandeji gumu. 
Nyota huyo aliandika kuwa anawajulisha mashabiki wake kuwa miezi michache inayokuja itakuwa migumu kwake kutokana na kuvunjika mguu. Hata hivyo aliwaondoa hofu mashabiki hao kwa kuwaambia kuwa atarudi akiwa imara zaidi zaidi ya alivyo sasa. Taarifa zitakuwa ni mbaya kwa meneja manuel Pellegrini wakati City wakitaka kutetea taji lao la ligi walilonyakuwa msimu uliopita.



No comments:

Post a Comment