Wednesday, July 23, 2014

RIBERY, MARTINEZ WAANZA MAZOEZI NA BAYERN.

WINGA mahiri wa kimataifa wa Ufaransa Franck Ribery na kiungo wa Hispania Javi Martinez wamejiunga na wachezaji wenzao jana wakirejea kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu nchini Ujerumani. Ribery aliikosa michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Brazil kutokana na majeruhi ya mgongo wakati Martinez yeye alikuwepo katika kikosi cha Hispania kilichotolewa katika hatua ya makundi baada ya kucheza mechi mbili. Ribery alijiunga na wachezaji wenzake wa Bayern na kufanya mazoezi na kikosi chote wiki iliyopita ikiwa ni dalili za kurejea katika hali yake ya kawaida. Meneja wa klabu ya Bayern Pep Guardiola bado hana wachezaji 10 kutoka katika kikosi chake cha kwanza kutokana na kupewa likizo ya ziada baada ya michuano ya Kombe la Dunia wakiwemo wachezaji sita wa kikosi cha Ujerumani. Bayern itaanza kutetea taji lake la ubingw awa Bundesliga Agosti 22 pale watakapoikaribisha Wolfsburg katika Uwanja wa Allianz Arena.

No comments:

Post a Comment