Wednesday, July 23, 2014

STOKE CITY YAMNASA BOJAN.

KLABU ya Stoke City imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Borjan Krkic kwa mkataba wa miaka minne. Bojan mwenye umri wa miaka 23 aliibuka katika kikosi cha kwanza cha Barcelona akiwa na umri wa miaka 16 lakini msimu uliopita alipelekwa kwa mkopo katika klabu ay Ajax Amsterdam ambako alifunga mabao manne katika mechi 24 alizocheza. Kocha wa Stoke Mark Hughes amesema amefurahishwa na usajili huo kwani anaamini nyota huyo bado ana kiwango cha kucheza katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Bojan ambaye ameitwa mara moja katika kikosi cha Hispania, ndiye mfungaji anayeongoza kwa mabao katika timu ya vijana akiwa amefunga zaidi ya mabao 400 huku akifunga mabao 26 katika kikosi cha kwanza cha Barcelona kati ya mwaka 2007 na 2011. Stoke tayari imeshawasajili Phil Bardsley, Steve Sidwell, Mame Biran Diouf na Dionatan Teixeira kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kwa msimu ujao.

No comments:

Post a Comment