Wednesday, July 23, 2014

PATRICK VIEIRA AWAONGOZA WACHEZAJI WA TIMU YA VIJANA YA MAN CITY KUTOKA UWANJANI BAADA YA KUFANYIWA UBAGUZI.

KIKOSI cha timu ya Manchester City cha wachezaji walio na umri chini ya miaka 21 kiliondoka uwanjani katika mchezo wa kirafiki nchini Croatia baada ya mmoja ya wachezaji kufanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi na timu pinzani. Mchezo huo dhidi ya klabu ya HNK Rijeka ulisitishwa baada ya tukio hilo lililomhusisha kiungo wa Ufaransa Seko Fofana. Taarifa ya City imedai kuwa uamuzi wa kuondoa kikosi hicho uwanjani na kuvunja mchezo kilifanywa na uongozi wakiongozwa kocha wa timu hiyo Patrick Vieira. Katika taarifa yao Rijeka walidai kuwa Vieira aliingia uwanjani kuzungumza kitu na mwamuzi na kisha kuchukua achezaji na kutoka katika uwanja uliokuwa umejaa mashabiki kwasababu ambazo anazijua mwenyewe. Hata hivyo City wamedai kuwa viongozi wa timu hiyo wanafanya kazi na waamuzi, waandaaji wa mechi na Chama cha Soka Croatia kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi kwa tukio hilo.

No comments:

Post a Comment