MENEJA wa klabu ya Napoli, Rafael Benitez amepuuzia mawazo kuwa kikosi chake kinaweza kutumia udhaifu wa Juventus baada ya Antonio Conte kujiuzulu wadhifa wa kuinoa klabu hiyo wiki iliyopita. Conte mwenye umri wa miaka 44 aliamua kusitisha mkataba wake wa kuinoa klabu hiyo Jumanne iliyopita baada ya kuingoza kushinda mataji matatu mfululizo katika kipindi cha miaka minne alichokuwa akifundisha. Pamoja na kuondoka ghafla kwa kocha huyo, Benitez amedai kuwa habari hizo hazijafungua milango kwa Napoli kutawala na kuongeza kuwa kocha mpya Massimiliano Allegri ataendelea kulinda hadhi ya klabu hiyo. Benitez amesema Juventus bado wataendelea kucheza kwa kiwango cha juu kwasababu Allegri ni kocha mzuri kama alivyokuwa Conte.
No comments:
Post a Comment