KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure amesema kuwa hana mpango wa kuondoka kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu na kudai ataendelea kuwepo hapo kwa msimu mwingine unaokuja. Toure aliiambia luninga ya Sky Sport kuwa mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wema kwake na kwa familia hivyo ameona ni bora abaki kwa ajili yao. Vyombo vya habari vimekuwa vikimhusisha kiungo huyo kuhamia katika vilabu mbalimbali toka wakala wake Dimitry Seluk alipoandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa nyota huyo hajatulia. Seluk alitoa madai kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast hakupewa utambulisho rasmi na klabu katika siku yake ya kuzaliwa wakati wa safari yao ya Abu Dhabu huku Toure mwenyewe akiunga mkono kauli hiyo. Toure amesema kwasasa mambo yote yako sawa na baada ya tetesi nyingi kuzungumziwa juu yake anaaka kufanya kitu kwa ajili ya mashabiki. Nyota huyo alijiunga na City akitokea Barcelona mwaka 2010 na haraka alijitengenezea jina na kua mchezaji tegemeo wa timu hiyo aliyoisaidia kushinda Kombe la FA mwaka 2011 na mataji mawili ya Ligi Kuu mwaka 2012 na 2014.
No comments:
Post a Comment