Wednesday, July 23, 2014

BLATTER AELEZA WASIWASI WAKE KUHUSU GAZA.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amefanya mazungumzo na kiongozi wa Chama cha Soka cha Palestina-PFA Jibril Rajub kuhusiana na vita vinavyoendelea katika ukanda wa Gaza. Blatter amesema wamekuwa na wasiwasi na hali ilivyo katika eneo hilo na wamesikitishwa kufahamu kuwa baadhi ya wanamichezo wamepoteza maisha na kilaani vikali vitendo hivyo vya vurugu. Blatter amesema kwa pamoja wanaungana kuomba na amani katika eneo na duniani kote kwa ujumla na kuongeza kuwa atakutana na Rajub kuzungumzia suala hilo wakati atakapokuwa katika mkutano wa Kimataifa wa Kamati ya Olimpiki utakaofanyka nchini Switzerland. Rajub ambaye mbali na kuingoza PFA pia ni kiongozi wa Kamati wa Olimpiki ya Palestina amesema anamshukuru Blatter kwa jitihada zake za kuendeleza na kuwekeza katika soka nchini humo pamoja na mambo magumu wanayokutana nayo. Rajub aliendelea kudai kuwa anaamini soka ndio njia pekee ya kuwaunganisha maadui wawili na amesikitishwa na roho za Wapalestina zilizoteketea kutokana na vurugu za sasa lakini ana imani amani itapatikana.

No comments:

Post a Comment