MASHINDANO ya Jumuiya ya Madola yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho huko jijini Glasgow, Scoland ambapo wanariadha mbalimbali wanatarajiwa kuonyeshana kazi katika michezo mbalimbali. Michuano ya mwaka huu ambayo ni ya 20 toka kuanzishwa kwake itajumuisha jumla ya wanariadha 4,500 kutoka mataifa 71 ambapo michezo 17 itashindaniwa ambapo kilele chake kitafikia Agosti 3 mwaka huu. Katika michuano hiyo Tanzania inawakilishwa na na wanariadha wapatao 39 ambao watashiriki michezo mbalimbali wakiwa huko ukiwemo riadha, ngumi, kurusha mishale, kuruka chini na mingineyo. Mojawapo ya wachezaji watano nyota ambao watashiriki michuano hiyo ni pamoja na bingwa anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 na 200 Usain Bolt kutoka Jamaica ambaye atashindana katika mbio za mita 400 kupokezana vijiti. Wengine ni Mo Farah wa Uingereza atakayeshindana katika mbio za mita 5,000 na 10,000, mwanadada Shelly-Ann Fraser-Pryce wa Jamaica atayeshindana mbio za mita 100 na mwendesha baiskeli Sir Bradley Wiggins atakayeshindana akiwa na timu ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment