Thursday, July 24, 2014

GLASGOW 2014: MO FARAH AJITOA MADOLA.

MWANARIADHA nyota na mshindi wa medali za dhahabu katika michuano ya olimpiki, Mo Farah amejitoa katika michuano ya Jumuiya ya Madola inayoendelea jijini Glasgow, Scotland baada ya kushindwa kupona maradhi yaliyokuwa yakimsumbua. Farah mwenye umri wa miaka 31 alishinda mbio za mita 5,000 na 10,000 katika michuano ya olimpiki iliyofanyika jijini London mwaka 2012 na alikuwa amepanga kukimbia katika umbali huo katika michuano hiyo. Hata hivyo pamoja na kujitoa ameamua kuendelea kubakia katika kambi yake ya mazoezi ili kujiweka fiti kwa ajili ya mashindano ya riadha ya Ulaya yatakayofanyika Agosti mwaka huu huko Zurich. Akihojiwa Farah amesema ulikuwa ni uamuzi mgumu kujitoa katika michuano hiyo lakini kilichomrudisha nyuma ni ugonjwa aliopata wiki mbili zilizopita kwani ingawa alikuwa akiendelea vyema na mazoezi lakini bado alikuwa akihitaji wiki chache zaidi ili kufikiwa kiwango alichokuwa nacho mwaka 2012 na 2013. Nyota huyo pamoja na kutamani medali ya Jumuiya ya Madola ili aweze kujumuisha na zile alizopata katika olimpiki na mshiandano ya dunia amesema mwili wake bado ulikuwa haiku fiti kwa ajili ya kukimbia ndio maana akajitoa.

No comments:

Post a Comment