Thursday, July 24, 2014

WAANDAMANAJI WA KIPALESTINA WAVAMIA UWANJA NA KUWAPIGA WACHEZAJI WA TIMU YA ISRAEL.

WAANDAMANAJI wa Kipalestina wamevuruga mchezo wa soka uliofanyika nchini Austria kati ya klabu ya Maccabi Haifa ya Israel na Lille ya Ufaransa. Mchezo huo uliokuwa wa kirafiki wa maandalizi ya msimu mpya wa ligi uliochezwa katika mji wa Bischofshofen ulisimamishwa wakati waandamanaji wa Kipalestina waliokuwa wakipeperusha bendera ya taifa walipovamia uwanjani. Polisi waliokuwepo eneo la tukio wamedai kuwa hakuna yeyote aliyejeruhiwa katika tukio hilo lililotokea karibu na mpira kumalizika. Israel wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kijeshi kuanzia Julai 8 mwaka huu wakidai kuwa na nia ya kuzuia mashambulizi ya roketi kutoka Gaza. Wapalestina wapatao 649, wanajeshi 32 wa Israel na raia watatu pia wa nchi hiyo wameuawa katika mapigano ambayo yamedumu kwa siku 15 sasa.

No comments:

Post a Comment