Thursday, July 24, 2014

DUNGA ACHUKUA NYOTA WENZAKE WA ZAMANI KUMSAIDIA KATIKA BENCHI LA UFUNDI.

KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Brazil, Dunga amemtaja Andrey Lopes kuwa msaidizi wake na pia kuwapa nafasi wachezaji wenzake wa zamani Taffarel na Mauro Silva nafasi katika benchi lake la ufundi. Lopes abaye sio maarufu sana aikuwa msaidizi wa Dunga wakati akiinoa klabu ya Internacional mwaka jana. Taffarel ambaye atakuwa kocha wa makipa alicheza sambamba na Dunga wakati waliposhinda Kombe la Dunia mwaka 1994 pamoja na Mauro Silva aliyekuwa kiungo ambaye Dunga amedai kuwa atamsaidia mahali na wakati atakaomhitaji. Katika benchi la ufundi la timu hiyo kuna majina 13 mapya yaliyoteuliwa ili kumsaidia dunga ambaye alitangazwa kuwa kocha mpya Jumanne. Kibarua cha kwanza cha Dunga ambaye uteuzi wake umepingwa na baadhi ya wadau wakidai alishindwa kuipeleka mbali nchi hiyo wakati akiifundisha katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010, utakuwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Colombia utakaochezwa jijini Miami Septemba 5 kabla ya kuivaa Ecuador jijini New Jersey siku nne baadae.

No comments:

Post a Comment