Wednesday, July 23, 2014

TYSON FURY SASA KUMALIZA HASIRA ZAKE KWA USTINOV BAADA YA KUMKOSA CHISORA.

BONDIA mahiri Tyson Fury anatarajiwa kupambana na Alexander Ustinov wa Belarus jijini Manchester Jumamosi hii kufuatia kuvunjika kwa pambano kati yake na Dereck Chisora. Chisora alijitoa katika pambano hilo baada ya kuvunjika mkono wake wa kushoto wakati akifanya mazoezi na Ustinov ndio alikuwa akifanya nae mazoezi wakati alipovunjika. Hii ni mara ya tatu kwa mapambano ya Fury mwenye umri wa miaka 25 kusitishwa baada ya mapambano mawili dhidi ya David haye nayo kusitishwa kutokana na bingwa huyo wa zamani wa dunia kujitoa. Ustinov mwenye umri wa miaka 37 ameshinda mapambano 29 kati ya 30 aliyocheza huku 21 kati ya hayo akishinda kwa knock-out.

No comments:

Post a Comment