Thursday, July 24, 2014

BORINI AUMIA WAKATI LIVERPOOL IKILALA MBELE YA ROMA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Liverpool Fabio Borini amepata majeruhi ya bega katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu dhidi ya Roma ya Italia. Katika mchezo huo beki wa zamani wa kimataifa wa Uingereza Ashley Cole alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Roma mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Fenway Park jijini Boston, Marekani. Liverpool walichabangwa bao 1-0 ambalo lilikuwa la kujifunga la Daniel Agger. Katika michezo mingine ya kirafiki ya kujipima nguvu iliyochezwa jana ni pamoja na Chelsea ambapo waling’ang’aniwa sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya RZ Pellets WAC huko Austria, Aston Villa ikiichabanga Dallas mabao 2-0 na Tottenham Hotspurs wakiinyesha kazi Toronto FC kwa kuifunga mabao 3-2. Michezo mingine ilikuwa Manchester United dhidi ya Los Angeles Galaxy ambapo kocha mpya Loius van Gaal alionyesha makali yake katika mchezo wa kwanza kushinda mabao 7-0 yaliyofungwa na Wayne Rooney, Ashley Young na Reece James ambao kila mmoja alifunga mawili na Danny Welberg. Kwa upande wa mabingwa wa Ligi Kuu Manchester City wao waliendeleza dozi zao kwa kuichapa Sporting Kansas City kwa mabao 4-1.

No comments:

Post a Comment