KLABU ya Manchester City imetangaza kumuongeza mkataba mpya wa miaka mitano kiungo mahiri wa kimataifa wa Ufaransa, Samir Nasri. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 sasa ataitumikia timu hiyo mpaka mwaka 2019 baada ya kuwa na msimu mzuri chini ya kocha Manuel Pellegrini ambapo alifunga mabao 11. Akihojiwa mara baada ya kutia saini mkataba huo Nasri amesema ana furaha kufanya hivyo kwani anataka kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi kirefu kijacho. Nasri alijiunga na City akitokea Arsenal mwaka 2011 na kucheza mechi 129 huku akifunga mabao 22 yakiwemo 11 aliyofunga msimu uliopita. Katika miaka mitatu ambayo ameichezea City mpaka sasa Nasri amefanikiwa kushinda taji la Ligi Kuu na Kombe la Ligi.
No comments:
Post a Comment