KLABU ya Queens Park Rangers-QPR imemuita golikipa wake Julio Cesar aliyekuwa akicheza kwa mkopo katika timu ya Toronto FC ya Marekani. Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 34 alihamia katika Ligi Kuu ya Marekani Februari mwaka huu baada ya kushindwa kupata muda wa kucheza chini ya kocha Harry Redknapp ambaye alikuwa akimpa nafasi Rob Green. Katika taarifa yake meneja mkuu wa Toronto waliwashukuru QPR kwa niaba ya klabu hiyo kwa kuwapa nafasi ya kumtumia Cesar huku pia wakimshukuru kipa huyo kwa mambo aliyowasaidia wakati akiwa hapo. Cesar alifanikiwa kucheza mechi zote za Kombe la Dunia nchini Brazil ambapo nchi yake waliokuwa wenyeji walipomaliza katika nafasi ya nne kufuatia kufungwa na Ujerumani katika nusu fainali na Uholanzi katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.
No comments:
Post a Comment