MENEJA wa zamani wa klabu ya Juventus, Antonio Conte amepuuzia taarifa kuwa anatarajia kuchukua nafasi ya Laurent Blanc katika klabu ya Paris Saint-Germain-PSG. Akihojiwa Conte amesema amesikia taarifa hizo kupitia vyombo vya habari wakati akiwa katika mapumziko yake kuwa amekuwa akifanya mawasiliano na PSG kwa ajili ya kwenda kuifundisha. Conte alikanusha taarifa hizo na kudai kuwa sio yeye wala wakala wake aliyefanya mazungumzo na klabu hiyo hivy hajui taarifa hizo wamezipata wapi. Gazeti moja la kila siku la michezo nchini Italia lilitoa taarifa jana kuwa Conte anakaribia kuchukua kibarua cha kuwafundisha mabingwa hao wa Ufaransa kwa madai kuwa wamepoteza imani na meneja wao wa sasa Blanc. Taarifa hizo pia zilikanushwa na PSG na kudai kuwa anaamini taarifa hiyo ilitoka kwa mwakilishi wa Conte ambaye alitaka kuweka shinikizo kwa vilabu vingine nchini Italia ambavyo amekuwa katika mazungumzo nao. Conte alijiuzulu nafasi yake ya ukocha katika timu ya Juventus wiki iliyopita baada ya kuifundisha kwa miaka mitatu na kushida mataji matatu mfululizo ya ligi, nafasi yake ilichukuliwa haraka na Massimiliano Allegri.
No comments:
Post a Comment