MABINGWA wa soka nchini Urusi, CSKA Moscow wamefanikiwa kutoka nyuma na kufanikiwa kushinda taji lao la sita la Super Cup jana baada ya kuitandika Rostov kwa mabao 3-1 huko Krasnodar. Mchezo huo wa ngao ya hisani kwa ajili ya ufunguzi wa pazia la ligi za nchi hiyo ambao hukutanisha bingwa wa Ligi Kuu na bingwa wa Kombe la Taifa ulichezwa kwa mara ya pili katika mji wa Krasnodar baada ya mara ya mwisho mechi kama hiyo kuchezwa mwaka 2011. Rostov ndio waliokuwa wa kwanza kuona lango la wapinzani wao katika dakika ya 37 kupitia kwa beki wa kimataifa wa Croatia Hrvoje Milic kabla ya CSKA nao kuzinduka kurejesha bao hilo na kuongeza mengine mawili yaliyowapa ushindi. Ligi Kuu nchini Urusi inatarajiwa kuanza rasmi katikati ya mwezi ujao kama ilivyo ratiba nyingi za ligi za Ulaya.
No comments:
Post a Comment