KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque amevunja ukimya kuhusu mustakabali wake na kubainisha kuwa amepanga kuendelea kuinoa timu hiyo moaka katika michuano ya Ulaya mwakani. Hispania walishindwa kutetea taji lao la Kombe la Dunia walilonyakuwa nchini Afrika Kusini mwaka 2010 kwa kutolewa katika hatua ya makundi katika michuano ya mwaka huu iliyofanyika nchini Brazil. Pamoja na kiwango cha chini cha timu hiyo walichoonyesha mwezi uliopita, Del Bosque amesisitiza kuwa hana mpango wa kuachia ngazi na amefurahi Shirikisho la Soka la Hispania kumuunga mkono. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 63 amesema wanaweza kufanya vizuri na kurejea katika mstari sahihi ili wajaribu kutetea taji lao la Ulaya katika michuano inayokuja. Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid alichukua nafasi ya Luis Aragones baada ya Hispania kunyakuwa taji la Ulaya mwaka 2008 na kuingoza kulitetea taji hilo mwaka 2012 sambamba na Kombe la Dunia mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment