Friday, July 18, 2014

UEFA YAWALIMA ADHABU SIMEONE NA ALONSO KWA UTOVU WA NIDHAMU.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA jana limefungia meneja wa klabu ya Atletico Madrid Diego Simeone na kiungo wa Real Madrid mechi moja kila mmoja kutokana na utovu wa nidhamu katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa uliochezwa Mei mwaka huu. Simeone alipewa adhabu hiyo kwa kuvamia uwanja mwishoni mwa mchezo huo huku akirushiana maneno na beki wa Madrid Rafael Varane. Kocha huyo atafungiwa kukaa katika nechi lake la ufundi katika mchezo unaofuata ambao watacheza mwanzoni mwa msimu mpya wa Ligi ya Mabingw Ulaya hatua ya makundi Septemba mwaka huu. Madrid walifanikiwa kuwafunga mahasimu wao hao mabao 4-1 baada ya muda wa nyongeza uliochezwa jijini Lisbon, Mei 24. Alonso naye alifungiwa kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu na anatarajiwa kukosa mchezo wa fainali ya Super Cup kati ya Madrid na bingwa wa Europa League Sevilla, Agosti 12 huko Cardiff. Atletico na Real Madrid nazo zilitozwa faini iliyotokana na kosa la wachezaji wa timu zote kupata kadi za njano zaidi ya tano katika mchezo huo ambapo Madrid walilimwa faini ya euro 18,000 kwa kupata kadi tano za njano wakati Atletico wao wamelimwa faini ya euro 21,000 kwa kupata kadi saba za njano.

No comments:

Post a Comment