MCHEZAJI nyota wa kimataifa wa zamani Uingereza, Rio Ferdinand amedai kuwa amekubali kusaini kuichezea klabu ya Queens Park Rangers sio kwasababu ya fedha. Ferdinand alikamilisha usajili wake jana ambao utamfanya kuitumikia timu hiyo ilipanda daraja msimu huu kwa msimu mmoja. Nyota huyo alitangaza kuondoka Manchester United Mei mwaka huu baada ya kuitumikia kwa miaka 12 huku akicheza mechi 454 ambapo mbali na tuzo zingine ameshinda mataji sita ya Ligi Kuu na moja la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya mwaka 2008. Akihojiwa Ferdinand amesema amepata ofa kutoka timu nyingi zenye hela nyingi lakini ameichagua QPR kwasababu bado anapenda kucheza katika Ligi Kuu na anafikiri ana uwezo wa kuisaidia timu hiyo kufikia malengo yake.
No comments:
Post a Comment