KLABU ya Flamengo yenye maskani yake jijini Rio de Janeiro imetangaza kumrejesha nyumbani mshambuliaji Eduardo da Silva kutoka Shakhtar Donetsk ya Ukraine. Nyota huyo wa kimataifa wa Croatia mzaliwa wa Brazil mwenye umri wa miaka 31 alianza soka lake katika klabu ya Dynamo Zagreb ya Croatia kabla ya kuhamia Arsenal mwaka 2007. Baada ya kucheza misimu miwili nchini Uingereza ambayo aliandamwa na majeruhi aliamua kuhamia Shakhtar mwaka 2010 na kufunga bao katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu huo dhidi ya Arsenal. Eduardo aliyeomba uraia wa Croatia mwaka 2002 amefanikiwa kucheza mechi za kimataifa za taifa hilo 60 lakini hakupata nafasi ya kucheza katika michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika nchini Brazil pamoja na kuitwa.
No comments:
Post a Comment