Friday, July 25, 2014

DRC YAJITOA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA KUANDAA AFCON 2019.

JAMHURI ya Kidemokrasi ya Congo-DRC imejiondoa katika kinyang’anyiro cha kugombea kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon mwaka 2019 bila ya kutoa sababu yoyote. Maofisa wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo wamedai kuwa ziara ya siku tano ya kikosi kazi kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika-CAFkwa ajili ya ukaguzi iliyokuwa ifanyike mwezi huu imesitishwa. Nchi zingine zinazogombea nafasi hiyo ni pamoja na Algeria, Cameroon, Guine, Ivory Coast na Zambia ambapo uamuzi unatarajiw akutolewa Septemba mwaka huu. Morocco ndio wanaotarajiwa kuandaa michuano hiyo mwakani wakifuatiwa na Libya mwaka 2017.

No comments:

Post a Comment