Friday, July 25, 2014

SINA MPANGO WA KUPIGANA TENA NA CHISORA - FURY.

BONDIA mahiri wa Uingereza, Tyson Fury amedai kuwa hataweza tena kupigana na hasimu wake katika ngumi za uzito wa juu Dereck Chisora baada ya bondia huyo kujitoa katika pambano lililokuwa lifanyike Jumamosi hii kutokana na majeruhi. Bondia huyo mwenye umri wa miaka 25 mzaliwa wa jiji la Manchester ambaye badala yake atapigana na Alexander Ustinov, amesema hadhani kama atakuja kupigana na tena na Chisora katika siku zijazo. Fury ilikuwa apambane na Chisora mwenye umri wa miaka 30 katika pambano ambalo mshindi angeweza kuvuzu kupata pambano la kugombania mkanda wa dunia wa WBO ambao unashikiliwa na Wladimir C. Fury ambaye alishuhudia mapambano yake mawili dhidi ya bondia David Haye yakisitishwa mwaka jana kutokana na majeruhi amesema anahisi mabondia hao huwa wanamuhofia hivyo wanafanya mazoezi ya nguvu sana yanayopelekea kupata majeruhi.

No comments:

Post a Comment