Thursday, July 24, 2014

MMOJA KATI YA WACHEZAJI SITA WA SHAKHTAR WALIOGOMEA UGENINI WAKIHOFU USALAMA WAO AREJEA NYUMBANI.

KIUNGO wa kimataifa wa Brazil, Fred amerejea katika klabu yake ya Shakhtar Donetski ambao ni mabingwa wa soka wa Ukraine baada ya timu hiyo kuhamisha makazi yake jijini Kiev. Fred mwenye umri wa miaka 21 alikuwa mmoja kati ya wachezaji sita waliogoma kurejea jijini Donetski kwasababu ya kuhofia usalama wao kutokana na mgogoro uliolikumba taifa hilo. Nyota mwingine wa kimataifa wa Brazil anayecheza nafasi ya ulinzi Ismaily anategemewa kurejea siku chache sijazo lakini Douglas Coast, Alex Teixeira, Dentinho na Fecundo bado hawajulikani kama watarejea. Ofisa Mkuu wa Shakhtar, Sergei Palkin amesema wengi kati yao wanaogopa hivyo wanajaribu kuwashawishi kwamba Ukraine ni salama na kama ikishindikana itabidi watumie mbinu zingine kuwarejesha. Wachezaji sita waligoma kuondoka Ufaransa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya klabu hiyo kucheza mechi yake kirafiki kutokana na mji wa Donetski kushikiliwa na waasi wa Urusi huku majeshi ya serikali ya Ukraine yakijaribu kuurejesha mji huo mikononi mwao.

No comments:

Post a Comment