Friday, July 25, 2014

PINTO ABWAGA MANYANGA COSTA RICA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Costa Rica, Jorge Luis Pinto ameamua kujizulu wadhifa wa kuinoa timu hiyo aliyoifikisha katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika nchini Brazil kwasababu ya kukataliwa kuchagua benchi lake la ufundi analohitaji. Kocha huyo raia wa Colombia mwenye umri wa miaka 61 amesema amaechukua uamuzi huo baada ya kuona hataweza kufanya kazi katika mazingira anayohitaji. Pinto aliongeza kuwa kutokana na majadilano ya muda mrefu kushindwa kupata muafaka ameamua kuachia nafasi hiyo ili kuwapisha wengine. Rais wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo, Eduardo Lee alithibitisha taarifa hizo na kumshukuru Pinto kwa kazi yake nzuri aliyofanya katika kipindi alichokuwa nao huku akimtakia kheri popote atakapoenda. Costa Rica walicheza mechi tano za Kombe la Dunia bila kufungwa kabla ya kutolewa na Uholanzi kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika mchezo war obo fainali.

No comments:

Post a Comment