Friday, July 25, 2014

GLASGOW 2014: TANZANIA YATUPA KARATA ZAKE NYINGINE LEO KATIKA MADOLA.

BONDIA wa Tanzania, Selemani Kidunda anapanda ulingoni baadae leo katika Michuano ya Jumuiya ya Madola inayoendelea jijini Glasgow, Scotland kwa kuzipiga na Mnigeria, Kehinde Ademuyiyiwa katika pambano la uzito wa Kilogram 69. Mabondia wote walipima uzito na afya jana kuanzia asubuhi kwa saa za Scotland na michuano ya ndondi itaanza leo hadi Agosti 2 katika ukumbi wa Secc (Hall 4A), Nahodha wa Tanzania, Selemani Kidunda akianza kupeperusha bendera ya taifa. Kesho bondia Nasser Mafuru atapigana na bondia wa Ghana Jessie Lartey katika pambano la uzito wa kilo 60 ilikifiatiwa baadae na pambano la Fabian Gaudence ataezipiga na Mmalawi Steven Thanki.  Michezo mingine ambayo itashirikisha wachezaji kutoka Tanzania kwa siku ya leo ni pamoja na kuogelea, Judo pamoja na mpira wa meza. Tanzania inawakilishwa na wanamichezo 39 katika michuano hiyo itakayoshindanishwa kwa siku 11 ambapo michezo watakayoshiriki ni pamoja na ngumi, riadha, judo, baisklei, mpira wa meza na kunyanyua uzito.

No comments:

Post a Comment