Monday, July 21, 2014

DROGBA AFIKIRIA KUREJEA CHELSEA.

MSHAMBULIAJI mkongwe Didier Drogba anafikiria kukubali ofa ya mkataba wa mwaka mmoja katika klabu ya Chelsea. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ambaye kwasasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Galatasaray aliondoka Stamford Bridge mwaka 2012 baada ya kushinda penati ya ushindi katika fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich. Wawakilishi wa Drogba wamesisitiza kuwa hakuna uamuzi wa mwisho uliotolewa na kuwa Chelsea ni moja ya klabu anazoweza kuchagua. Lakini mazungumzo bado yanaendelea na mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 anaweza kufanya uamuzi wa kurejea Chelsea wiki hii.

No comments:

Post a Comment